Shirika la Uchumi na Maendeleo la jiji la Dar es salaam ,Linaendelea na mradi wa upimaji wa viwanja kwanye eneo lake la Mabwepande jijini Dar es salaam
Kutokana na Vikao na mikutano mbali mbali ya Viongozi na wanachi wa Mabwepande, Yamefikiwa Makubaliano ya Bei mpya ambayo ni TSH 3000 Kwa mita moja ya mraba.
Aidha wananchi wote ambao teyari Wamekwisha patiwa “control numbers” wanahimizwa kufanya malipo ya Viwanja vyao Mapema kupitia Tawi lolote la TCB(Tanzania Commercial bank) zamani Benki ya Posta.
Wale ambao bado hawajapata Control numbers wameombwa kufika ofisi ya Serikali ya Mtaa kuchukua Control numbers zao . Au wasiliana na Shirikika kupitia Anuani ifuatayo.
Shirika la Uchumi la Maendeleo la Jiji la Dar es salaam
Mtaa wa Msimbazi/Mhonda
S.l.p 1330
Dar es salaam.
Simu: +255(0)222180842
Barua pepe: info@ddc.co.tz






Leave a Comment